Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 10/15 kur. 8-9
  • Upapa Je! Ulianzishwa na Kristo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Upapa Je! Ulianzishwa na Kristo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Papa Ndiye “Mrithi wa Mtakatifu Petro”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Je, Petro alikuwa Papa wa Kwanza?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Alijifunza Kusamehe Kutoka kwa Bwana Wake
    Igeni Imani Yao
  • Acheni Tuishike Sana Imani Yetu Yenye Thamani!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 10/15 kur. 8-9

Upapa Je! Ulianzishwa na Kristo?

“KATIKATI ya Petro, Askofu wa Roma wa kwanza, na papa wetu wa sasa, John Paul 2, kuna mstari wa maaskofu wakuu unaoenea kwa kipindi kirefu—kwa kweli, wao ni zaidi ya 260.” Ndivyo asemavyo Anthony Foy mtawa-mume Mkatoliki katika The Southern Cross, gazeti la Kikatoliki litokalo kila juma kusini mwa Afrika Kusini. Yeye aendelea hivi: “Mstari huo wa mapapa usiovunjika ndio ambao tunaelekezea kwa hakika, tunapoulizwa tuthibitishe kwamba Kanisa la Katoliki lilianzishwa na Yesu Kristo.”

Je! yaweza kusemwa kwa hakika kwamba mstari huo mrefu wa mapapa ulianza na mtume Petro? Kulingana na theolojia ya Kikatoliki, mapapa wanne, Lino, Anakleto, Clement 1, na Evaristo, wanasemwa kuwa waandamizi wa Petro hadi mwaka wa 100 W.K. Ni kweli Biblia hutaja Mkristo aitwaye Lino aliyeishi Roma. (2 Timotheo 4:21) Hata hivyo, hakuna lolote linalodokeza kwamba Lino, au mtu yeyote mwingine, alikuwa mwandamizi wa kipapa wa Petro. Mtume Yohana, aliyeandika vitabu vitano vya Biblia katika mwongo wa mwisho wa karne ya kwanza, hakufanya rejezeo lolote kwa yeyote kati ya wale wanaoitwa eti waandamizi wa Petro wanaotajwa juu. Kwa kweli, ikiwa kulikuwako mwandamizi wa Petro, je, Yohana mwenyewe asingalikuwa chaguo lililo bora zaidi?

Kuhusu lile dai kwamba Petro ndiye aliyekuwa askofu wa kwanza wa Roma, hakuna uthibitisho wowote kwamba yeye hata alitembelea jiji hilo. Kwa kweli, Petro mwenyewe ataarifu kwamba aliandika barua yake ya kwanza kutoka Babuloni. (1 Petro 5:13) Hoja ya Kikatoliki kwamba Petro alitumia “Babuloni” kuwa rejezeo la kifumbo kwa Roma haina msingi. Babuloni halisi ilikuwako katika siku ya Petro. Isitoshe, Babuloni ilikuwa na jumuiya kubwa ya Kiyahudi. Kwa kuwa Yesu alimpa Petro mgawo wa kukazia kuhubiri kwake hasa kwa Wayahudi waliotahiriwa, kwa ujumla ni jambo la akili kuamini kwamba Petro alitembelea Babuloni kwa kusudi hilo.—Wagalatia 2:9.

Ona pia, kwamba Petro hakujirejezea mwenyewe kamwe kuwa mwenye hali iliyo zaidi ya mmoja wa mitume wa Kristo. (2 Petro 1:1) Hamna mahali popote katika Biblia aitwapo “Baba Mtakatifu,” “Askofu Mkuu Zaidi,” au “Papa” (Kilatini, papa, neno lenye shauku kwa “Baba”). Badala ya hivyo, yeye alifuata kwa unyenyekevu maneno ya Yesu kwenye Mathayo 23:9, 10: “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.” Petro hakukubali heshima ya kiibada. Korne-lio akida Mroma ‘alipomwangukia miguu, na kumsujudia . . . , Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.’—Matendo 10:25, 26.

Kuhusu wale 260 wanaoitwa mapapa bila uthibitisho, padri Foy akiri hivi: “Wengi wao hawakustahili cheo chao cha juu.” Ili kujaribu kutetea hilo, New Catholic Encyclopedia yataarifu hivi: “Jambo la maana sana kwa sababu ya makusudi ya serikali lilikuwa cheo, wala si tabia ya binafsi ya papa mmoja mmoja. Yeye kibinafsi angeweza kuwa mtakatifu, mtu asiye mwema wala mbaya, au hata mtu mbaya sana.” Lakini je, wewe unaamini kwamba Kristo angetumia wanaume kama hao kumwakilisha?

Kwa vyovyote vile, dai la kwamba upapa ulianzishwa na Yesu haliungwi mkono na Biblia hata kidogo. Kulingana na Encyclopedia of Religion, hata wanachuo Wakatoliki wa ki-siku-hizi hukubali kwamba “hakuna uthibitisho wa kibiblia wa moja kwa moja kwamba Yesu alisimamisha upapa kuwa cheo cha kudumu ndani ya kanisa.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki