Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 9/1 uku. 3
  • Tafsiri za Biblia za Afrika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tafsiri za Biblia za Afrika
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Kitabu “Kisemacho” Lugha Zilizo Hai
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
  • Hatua Muhimu Katika Kutokeza Biblia za Lugha za Kiafrika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Tafsiri ya New World Translation Inathaminiwa na Mamilioni ya Watu Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 9/1 uku. 3

Tafsiri za Biblia za Afrika

Tafsiri za mapema zaidi za Biblia nzima katika lugha moja ya Afrika zilifanywa katika Misri. Zikijulikana kuwa tafsiri za Kikoptiki, zinadhaniwa kuwa zenye tarehe kutoka karne ya tatu au ya nne W.K. Karibu karne tatu baadaye, Biblia ilitafsiriwa katika lugha ya Kiethiopia.

Mamia ya lugha ambazo hazikuwa zimeandikwa zilizosemwa kusini mwa Ethiopia na Sahara zilihitaji kungojea kuwasili kwa wamishonari katika karne ya 19. Katika 1857 hatua ya maana ilifikiwa wakati Robert Moffat alipokamilisha tafsiri ya Biblia katika Kitswana, lugha ya kusini mwa Afrika. Pia aliichapisha katika sehemu-sehemu kwenye matbaa ya mkono. Hiyo ilikuwa Biblia kamili ya kwanza kuchapishwa katika Afrika na ilikuwa ndiyo tafsiri kamili ya kwanza katika lugha ya Afrika ambayo haikuwa imeandikwa kabla ya wakati huo. Kwa kupendeza, Moffat alitumia jina la kimungu Yehova katika tafsiri yake. Katika tafsiri ya 1872 iliyotangazwa kwa chapa na Sosaiti ya Biblia ya Uingereza na Nchi za Kigeni, jina Yehova hutumiwa katika taarifa kuu zilizotolewa na Yesu kama zilivyorekodiwa kwenye Mathayo 4:10 na Marko 12:29, 30.

Kufikia 1990 Biblia nzima ilikuwa imetafsiriwa katika lugha za Afrika 119, sehemu zayo zikipatikana katika lugha nyinginezo 434.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki