Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 3/15 kur. 21-23
  • Yehova—Mpenda Uadilifu na Haki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova—Mpenda Uadilifu na Haki
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Rehema na Haki ya Yehova
  • Iga Haki ya Yehova
  • Panda Mbegu kwa Uadilifu
  • Yehova—Chanzo cha Haki na Uadilifu wa Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Mwige Yehova—Dhihirisha Haki na Uadilifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • “Njia Zake Zote Ni Haki”
    Mkaribie Yehova
  • Haki Karibuni kwa Ajili ya Mataifa Yote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 3/15 kur. 21-23

Yehova—Mpenda Uadilifu na Haki

MSICHANA mmoja mchanga katika Sarajevo ajiuliza mwenyewe ni kwa nini watoto katika jiji lake wanateseka sana. “Hatujafanya lolote. Sisi hatuna hatia,” yeye asema. Akina mama waliofadhaika sana wa Argentina wamefanya maandamano kwenye uwanja fulani katika Buenos Aires kwa miaka 15 hivi, wakilalamika kwa sababu ya kupotea kwa wana wao. Mwafrika aitwaye Emmanuel, ambaye mama yake na dada zake watatu waliuawa kinyama wakati jeuri ya kikabila ilipoanza, asisitiza: “Lazima kila mmoja apate hukumu astahiliyo . . . Twataka haki.”

Haki ni mojawapo sifa kuu za Yehova Mungu. “Njia zake zote ni haki,” yasema Biblia. Kwelikweli, Yehova ni “mpenda uadilifu na haki.” (Kumbukumbu la Torati 32:4; Zaburi 33:5, NW) Ili kumjua Mungu vizuri, lazima tufahamu haki yake na tujifunze kuiiga.—Hosea 2:19, 20; Waefeso 5:1.

Huenda maoni yetu juu ya haki yameathiriwa na yale ambayo wanadamu hufikiri sifa hii humaanisha. Katika sehemu fulani ulimwenguni, haki hufananishwa na mwanamke aliyefunikwa macho anayebeba upanga na mizani. Haki ya kibinadamu yapaswa kuwa isiyopendelea, yaani, haioni utajiri wala kuvutiwa. Lazima ipime kwa uangalifu kwenye mizani kuwa na au kukosa hatia kwa mshtakiwa. Kwa kutumia upanga wayo, haki yapaswa ilinde wasio na hatia na kuwaadhibu wakosaji.

Kitabu Right and Reason—Ethics in Theory and Practice husema kwamba “haki yahusianishwa na sheria, wajibu, haki za watu, na masharti mbalimbali, nayo hutoa hukumu bila kupendelea na kwa yule aistahiliye.” Lakini haki ya Yehova hupita hiyo. Twaweza kuona hilo kwa kufikiria matendo na sifa za Yesu Kristo, afananaye sana na Baba yake wa kimbingu.—Waebrania 1:3.

Maneno ya Isaya 42:3 yalitumiwa kumhusu Yesu na mwandikaji wa Gospeli Mathayo, aliyetaarifu: “Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima, hata ailetapo hukumu [“haki,” NW] ikashinda.” Yesu aliwatangazia watu waliokuwa kama mwanzi uliopondeka uliokuwa umekunjwa na hata kukanyagwa-kanyagwa ujumbe wenye kufariji. Walikuwa kama utambi utokao moshi, kana kwamba walikuwa karibu kuzimika. Badala ya kuvunja mwanzi uliopondeka na kuzima utambi utokao moshi kwa njia ya kitamathali, Yesu aliwahurumia waliokuwa wakiteseka, akawafundisha na kuwaponya, na akawafafanulia waziwazi haki ya Yehova Mungu. (Mathayo 12:10-21) Kama unabii wa Isaya ulivyotabiri, haki ya aina hiyo ilitokeza tumaini.

Rehema na Haki ya Yehova

Rehema ni sehemu kubwa ya haki ya Mungu. Hilo lilionekana wazi wakati Yesu alipokuwa duniani. Yeye aliwakilisha kikamilifu viwango vya Mungu vya haki na uadilifu. Hata hivyo, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi walitafuta kupata uadilifu kwa kufuata kanuni kali za sheria kikamili—nyingi zazo zikiwa zao wenyewe. Haki yenye kufuata sheria mno mara nyingi iliondolea mbali rehema. Mabishano mengi kati ya Yesu na Mafarisayo yalikuwa juu ya suala hili: Haki na uadilifu za kweli ni nini?—Mathayo 9:10-13; Marko 3:1-5; Luka 7:36-47.

Yesu alitoa kielezi cha njia ya kuwatendea wengine kwa haki na uadilifu. Wakati mmoja mtu aliyeijua Sheria vizuri alimwuliza Yesu kilichohitajika ili mtu aurithi uhai udumuo milele. Akimjibu Yesu alimwuliza swali na kumpongeza alipojibu kwamba sheria mbili zilizo za maana sana ni kumpenda Mungu kwa moyo, nafsi, akili, na nguvu zote na kumpenda jirani kama unavyojipenda mwenyewe. Huyo mtu kisha akauliza: “Jirani yangu ni nani?” Yesu alijibu kwa kutumia kielezi cha Msamaria mwenye ujirani.—Luka 10:25-37.

Uadilifu na haki yenye rehema ya Yehova zilionyeshwa wazi katika kielezi cha Yesu cha Msamaria. Kwa kumsaidia bila ubinafsi mtu aliyekuwa amejeruhiwa asiyemjua, huyo Msamaria alifanya jambo lililofaa, la haki, na lenye kujaa rehema. Yesu mwenyewe alionyesha roho hiyohiyo alipokuwa duniani. Alikuwa mwadilifu na mwenye haki. Zaidi ya hayo, alitoa uhai wake kwa ajili ya watu wenye uhitaji, wanadamu wenye dhambi na wasio wakamilifu waliokumbwa na kuteseka, magonjwa, na kifo. Mtume Paulo alihusianisha uadilifu na ule uandalizi wa fidia. Yeye aliandika: “Kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki [au, “tendo moja la uadilifu,” New World Translation of the Holy Scriptures—With References, kielezi chini] watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.” (Warumi 5:18) Hilo “tendo moja la uadilifu” lilikuwa njia ya Mungu ya kuokoa wanadamu watiifu kutoka kwa matokeo yenye msiba ya dhambi ya Adamu, ambayo hawakuhusika nayo moja kwa moja.

Haki ya Mungu ilitafuta kukomboa wanadamu wenye dhambi na wakati uleule kudumisha kanuni za uadilifu. Kupuuza dhambi kungekuwa kukosa haki na upendo, kwa kuwa kungeendekeza uvunjaji wa sheria. Kwa upande ule mwingine, ikiwa haki ya Mungu ingekuwa tu kuthawabisha au kuhukumu, wanadamu wangekosa tumaini. Kulingana na Biblia, “mshahara wa dhambi ni mauti” na “hakuna mwenye haki [“uadilifu,” NW] hata mmoja.” (Warumi 3:10; 6:23) Kwa gharama kubwa sana kwake mwenyewe na kwa Mwanaye mpendwa, Yehova aliandaa dhabihu ya kuridhisha kwa ajili ya dhambi.—1 Yohana 2:1, 2.

Fidia huonyesha kwamba haki ya kimungu huambatana na upendo wenye kanuni (Kigiriki, a·gaʹpe). Kwelikweli, haki ya Mungu ni kule kutekelezwa kwa kanuni zake za uadilifu—wonyesho wa viwango vyake vya kiadili. Kwa hivyo, unapodhihirishwa na Mungu, a·gaʹpe ndio upendo ambao haki ya kimungu hutegemea. (Mathayo 5:43-48) Hivyo, tukifahamu haki ya Yehova vizuri, tutakuwa na tumaini kamili kwa maamuzi yake ya kihukumu. Akiwa “Mhukumu ulimwengu wote,” sikuzote yeye hufanya lililo sawa.—Mwanzo 18:25; Zaburi 119:75.

Iga Haki ya Yehova

Biblia hutuhimiza “tuwe waigaji wa Mungu.” (Waefeso 5:1, NW) Hili lamaanisha kuiga haki na upendo wake. Hata hivyo, kwa kuwa hatujakamilika, njia zetu si za juu kama za Yehova Mungu. (Isaya 55:8, 9; Ezekieli 18:25) Twaweza basi kuwaje wapenda uadilifu na haki? Kwa kuvaa “utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki [“uadilifu,” NW] na utakatifu [“uaminifu-mshikamanifu,” NW] wa kweli.” (Waefeso 4:24) Ndipo tutapenda apendayo Mungu na kuchukia ayachukiayo. ‘Uadilifu wa kweli’ huepuka ujeuri, ukosefu wa adili, ukosefu wa usafi, na uasi-imani, kwa kuwa haya huchafua kilicho kitakatifu. (Zaburi 11:5; Waefeso 5:3-5; 2 Timotheo 2:16, 17) Haki ya kimungu vilevile hutuchochea kuonyesha upendezi wa kweli kwa wengine.—Zaburi 37:21; Warumi 15:1-3.

Zaidi ya yote, tukifahamu jinsi haki ya Mungu ina rehema, hatutaelekea kuwahukumu ndugu na dada wa kiroho. Twaweza kuwafahamuje kama awafahamuvyo Yehova? Je, hatungewahukumu kulingana na maoni yetu wenyewe yenye ubaguzi? Kwa sababu hiyo, Yesu alionya: “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.” (Mathayo 7:1-5) Kutambua kwa unyofu kutokamilika kwetu wenyewe kutatuzuia tusitoe hukumu ambazo Yehova angeziona kuwa zisizo na uadilifu.

Wazee waliowekwa rasmi wana wajibu wa kuhukumu katika kesi za kosa zito. (1 Wakorintho 5:12, 13) Wafanyapo hivyo, wao hukumbuka kwamba haki ya Mungu huonyesha rehema iwezekanapo. Ikiwa hakuna msingi wa rehema—kama katika kisa cha watenda dhambi wasiotubu—hiyo haiwezi kuonyeshwa. Lakini wazee hawafukuzi wakosaji kutoka kutanikoni kwa sababu ya kisasi. Wao hutumaini kwamba tendo la kutenga na ushirika litamfanya apate kurudia fahamu zake. (Linganisha Ezekieli 18:23.) Chini ya ukichwa wa Kristo, wazee hufuatia haki, na hilo hutia ndani kuwa kama “mahali pa kujificha na upepo.” (Isaya 32:1, 2) Hivyo ni lazima waonyeshe kutopendelea na kuwa wenye kukubali sababu.—Kumbukumbu la Torati 1:16, 17.

Panda Mbegu kwa Uadilifu

Tuungojeapo ulimwengu mpya wenye uadilifu wa Mungu, ili kupata kibali cha kimungu ni lazima ‘tutafute haki [“uadilifu,” NW].’ (Sefania 2:3; 2 Petro 3:13) Wazo hili laonyeshwa vizuri katika maneno haya, yapatikanayo kwenye Hosea 10:12: “Jipandieni [“mbegu,” NW] katika haki [“uadilifu,” NW], vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki [“uadilifu,” NW].”

Katika maisha zetu za kila siku, tuna fursa nyingi za ‘kujipandia mbegu katika uadilifu,’ jinsi tu Yesu alivyoonyesha kupitia kielezi chake cha Msamaria mwenye ujirani. Yehova atahakikisha kwamba ‘tutavuna kwa fadhili.’ Tukiendelea kutembea katika “njia ya haki,” tutaendelea kupokea maagizo katika uadilifu chini ya utawala wa Ufalme. (Isaya 40:14, NW) Muda uzidipo kupita, bila shaka tutang’amua hata zaidi kwamba Yehova ni mpenda uadilifu na haki.—Zaburi 33:4, 5.

[Picha katika ukurasa wa 23]

Msamaria mwenye ujirani alifananisha haki ya Yehova

[Picha katika ukurasa wa 23]

Yesu aliwahurumia watu wenye kuteseka, waliokuwa kama mwanzi uliopondeka

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki