Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 10/15 uku. 3
  • Jitihada Yetu ya Kuishi Muda Mrefu Zaidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jitihada Yetu ya Kuishi Muda Mrefu Zaidi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Tumaini Gani kwa Maisha Marefu Zaidi?
    Amkeni!—1995
  • Jitihada za Mwanadamu za Kupambana na Kifo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Watu Wanaweza Kuishi Muda Mrefu Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Jitihada za Kurefusha Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 10/15 uku. 3

Jitihada Yetu ya Kuishi Muda Mrefu Zaidi

“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.” —Ayubu 14:1, 2.

HATA leo ni wachache wawezao kupinga maneno hayo kuhusu ufupi wa maisha, ingawa yaliandikwa miaka ipatayo 3,500 iliyopita. Sikuzote watu hawaridhiki kufurahia upeo wa maisha kwa muda mfupi tu, kisha kuzeeka na kufa. Hivyo, njia za kurefusha maisha zimeongezeka katika historia yote.

Wakati wa Yobu Wamisri walikula mapumbu ya wanyama katika jitihada ambazo hazikufua dafu za kurudia ujana wao. Lengo moja kuu la tiba ya kurefusha maisha ya enzi za kati lilikuwa kutokeza dawa ambayo ingeweza kurefusha maisha. Waliofuatia tiba ya kurefusha maisha waliamini kwamba dhahabu iliyotokezwa na wanadamu ingesababisha uhai usioweza kufa na kwamba kulia sahani za dhahabu kungerefusha maisha. Wachina wa kale waliofuata dini ya Tao walifikiri kwamba wangeweza kugeuza maumbile ya mwili kwa kutumia mbinu kama kutafakari, mazoezi ya kupumua, na utaratibu maalum wa kula na hivyo kufikia hali ya kutoweza kufa.

Mvumbuzi Mhispania aitwaye Juan Ponce de León anajulikana kuwa alitafuta kwa udi na uvumba chemchemi ya ujana. Daktari fulani wa karne ya 18 alipendekeza katika kitabu chake, Hermippus Redivivus, kwamba mabikira wachanga wawekwe katika kijumba wakati wa masika na pumzi zao zikusanywe katika chupa na kutumiwa kama dawa ya kurefusha maisha. Ni wazi kwamba hakuna hata moja ya mbinu hizo iliyofanikiwa.

Leo, miaka ipatayo 3,500 baada ya Musa kuandika maneno hayo ya Yobu, mwanadamu ametembea kwenye mwezi, akabuni magari na kompyuta, na kuchunguza atomu na chembe. Hata hivyo, licha ya hatua hizo zote za kitekinolojia, bado ‘siku zetu za kuishi si nyingi, nasi tumejaa taabu.’ Ni kweli kwamba katika nchi zilizositawi muda wa kuishi umeongezeka sana katika karne iliyopita. Lakini hali hiyo imetokana hasa na maendeleo ya kitiba, hatua za usafi zifaazo, na chakula kifaacho zaidi. Kwa mfano, tangu katikati ya karne ya 19 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, muda wa kuishi nchini Sweden umeongezeka kutoka miaka 40 hadi miaka 75 kwa wanaume, na kutoka miaka 44 hadi 80 kwa wanawake. Lakini jambo hilo lamaanisha kwamba tamaa ya mwanadamu ya kuishi muda mrefu zaidi imetoshelezwa?

La, kwa sababu ingawa katika nchi fulani watu huishi wakawa wazee, maneno haya yaliyoandikwa na Musa miaka mingi iliyopita yangali yanatumika: “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, na ikiwa tuna nguvu miaka themanini . . . , maana [za]pita upesi tukatokomea mara.” (Zaburi 90:10) Je, kutakuwa na mabadiliko hivi karibuni? Je, mwanadamu ataweza kuishi kwa muda mrefu zaidi? Makala ifuatayo itazungumzia maswali hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki