Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 7/1 kur. 3-4
  • Je,Unaweza Kupata Amani ya Akili?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je,Unaweza Kupata Amani ya Akili?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Walitafuta Amani ya Akili
  • Unaweza Kupata Wapi Amani ya Akili?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Je, Unaweza Kupata Amani Katika Ulimwengu Huu Wenye Misukosuko?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Yohana 14:27—“Amani Nawaachieni”
    Mistari ya Biblia Yafafanuliwa
  • Amani​—Unaweza Kuipataje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 7/1 kur. 3-4

Je,Unaweza Kupata Amani ya Akili?

Mnamo mwaka wa 1854, mwandishi Mmarekani, Henry Thoreau, aliandika hivi: “Watu wengi wanaishi maisha yasiyo na tumaini bila kulalamika.”

Yaonekana kwamba katika wakati wake watu wengi hawakuwa na amani ya akili. Hata hivyo, hayo ni mambo ya miaka 150 iliyopita. Je, hali ni tofauti leo? Au hali bado iko kama alivyosema Thoreau? Namna gani wewe binafsi? Je, umeridhika, una amani? Au je, umekosa usalama, una shaka juu ya wakati ujao, ‘umekata tumaini bila kulalamika,’ kulingana na maneno ya Thoreau?

KWA kusikitisha, kuna mambo mengi ulimwenguni yanayowanyima watu amani ya akili. Ebu tutaje machache tu. Katika nchi nyingi ukosefu wa kazi ya kuajiriwa na mapato ya chini husababisha umaskini na hali mbaya ya uchumi. Katika nchi nyingine watu wengi hutumia nguvu nyingi wakitafuta mali na vitu vya kimwili. Ingawa hivyo, mara nyingi maisha ya kushindana wanayoishi huwaletea wasiwasi, si amani. Magonjwa, vita, uhalifu, ukosefu wa haki, na uonevu pia huwanyima watu amani.

Walitafuta Amani ya Akili

Watu wengi hawako tayari kuvumilia jinsi hali ilivyo ulimwenguni. Antônioa alikuwa kiongozi wa wafanyakazi katika kiwanda kikubwa huko São Paulo, Brazili. Akitumaini kuboresha hali za maisha, alishiriki katika mateto na maandamano, lakini mambo hayo hayakumletea amani ya akili.

Wengine hutumaini kwamba ndoa itawaletea kiasi fulani cha utulivu maishani, lakini huenda wakatamauka. Marcos alikuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio. Alijiingiza katika siasa, akawa meya wa jiji fulani lenye viwanda. Hata hivyo, hali nyumbani kwake iliharibika kabisa. Watoto wake walipoondoka nyumbani, yeye na mke wake walitengana kwa sababu hawangeweza kupatana.

Gerson, aliyekuwa mtoto mwenye kurandaranda mitaani huko Salvador, Brazili, alitaka maisha ya kujasiria. Alisafiri bila kusudi kutoka jiji hadi jiji, akiomba lifti kwa madereva wa malori. Muda si muda akawa mraibu wa dawa za kulevya, akinyang’anya watu ili kugharimia zoea hilo baya. Polisi walimkamata mara kadhaa. Hata hivyo, Gerson alitamani amani ya akili japo alikuwa mchokozi na mjeuri. Je, angeweza kuipata?

Mama ya Vania alikufa Vania akiwa bado mchanga, hivyo akachukua madaraka ya nyumbani, pamoja na kumtunza dada yake mgonjwa. Vania alienda kanisani lakini alihisi ameachwa na Mungu. Kwa hakika yeye hakuwa na amani ya akili.

Mwingine ni Marcelo. Marcelo alitaka tu kujifurahisha. Alipenda kwenda karamuni pamoja na vijana wengine—kucheza dansi, kunywa pombe, na kutumia dawa za kulevya. Siku moja alipigana na kijana mmoja na kumjeruhi. Baadaye, alijutia sana tendo hilo, akasali kwa Mungu amsaidie. Yeye pia alitaka amani ya akili.

Mambo hayo yanaonyesha hali fulani zinazoweza kuharibu amani ya akili. Je, kuna njia yoyote ambayo yule kiongozi wa wafanyakazi, yule mwanasiasa, yule mtoto mwenye kurandaranda mitaani, yule binti mwenye kufanya kazi kupita kiasi, na yule mwenda-karamuni wangeweza kupata amani ya akili waliyotafuta? Je, yaliyowapata yanatufunza jambo lolote? Jibu kwa maswali yote mawili ni ndiyo, kama tutakavyoona katika makala ifuatayo.

[Maelezo ya Chini]

a Majina mengine yamebadilishwa.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Je, unatamani sana amani ya akili?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki