Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 8/15 uku. 30
  • Je, Unakumbuka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unakumbuka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Tafsiri ya Complutensian Polyglot—Ni Kifaa Muhimu Katika Utafsiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Tafsiri ya Royal Bible—Hatua Kubwa Katika Usomi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Somo Kuhusu Kiburi na Unyenyekevu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 8/15 uku. 30

Je, Unakumbuka?

Je, umefurahia kusoma matoleo ya hivi karibuni ya Mnara wa Mlinzi? Ona kama unaweza kujibu maswali yafuatayo:

• Tafsiri ya Complutensian Polyglot ni nini, na kwa nini ilikuwa muhimu?

Ilikuwa tafsiri ya Biblia iliyonukuliwa katika lugha nyingi ambazo zilipangwa katika safu mbalimbali. Pia ilikuwa tafsiri bora zaidi iliyopatikana wakati huo katika Kiebrania, Kigiriki, Kilatini, na sehemu fulani katika Kiaramu. Kutafsiriwa kwa Biblia hiyo kulikuwa hatua kubwa katika kutokeza maandishi sahihi ya lugha za awali.—4/15, ukurasa wa 28-31.

• Wanadamu wanawezaje kumfanya Mungu ashangilie?

Kwa kuwa Yehova ni mtu halisi aliye hai, yeye anaweza kufikiri, kutenda, na kuhisi. Yeye ni “Mungu mwenye furaha,” naye hufurahia kutimiza kusudi lake. (1 Timotheo 1:11; Zaburi 104:31) Kadiri tunavyozidi kuelewa hisia za Mungu, ndivyo tunavyozidi kufahamu mambo tunayoweza kufanya ili kuufurahisha moyo wake.—5/15, ukurasa wa 4-7.

• Kwa nini Daudi alimruhusu mke wake Mikali aweke sanamu ya terafimu?

Mfalme Sauli alipopanga njama ya kumuua Daudi, Mikali alimsaidia kutoroka, huku akilaza sanamu kwenye kitanda, ambayo yaelekea ilikuwa na umbo la mwanadamu. Huenda aliweka terafimu kwa kuwa moyo wake haukuwa kamili kumwelekea Mungu. Ama Daudi hakujua kuhusu sanamu hiyo ama aliivumilia tu kwa sababu Mikali alikuwa binti ya Mfalme Sauli. (1 Mambo ya Nyakati 16:25, 26)—6/1, ukurasa wa 29.

• Ni nini lililokuwa jambo kuu katika maagizo ya Mungu kuhusu damu?

Kupitia mambo ambayo Mungu alisema baada ya Gharika katika Sheria ya Musa, na katika lile agizo kwenye Matendo 15:28, 29, yeye alikazia dhabihu iliyohusisha damu ya Yesu iliyomwagwa. Ni kupitia damu hiyo tu tunaweza kusamehewa dhambi na kuwa na amani pamoja na Mungu. (Wakolosai 1:20)—6/15, ukurasa 14-19.

• Ni miujiza mingapi ya Yesu inayotajwa katika Biblia?

Masimulizi ya Injili yanataja miujiza ya Yesu ipatayo 35. Lakini hesabu kamili ya miujiza ya Yesu, kutia ndani ile ambayo haikutajwa, haijulikani. (Mathayo 14:14)—7/15, ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki