Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp19 Na. 1 uku. 3
  • Mungu Ni Nani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Ni Nani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Unaweza Kufanya Nini Ili Umjue Mungu Kibinafsi?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Je, Unamfahamu Baba Yako wa Mbinguni?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Mungu Ni Nani?
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Ukweli Kumhusu Mungu
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
wp19 Na. 1 uku. 3
Mwanamume anastaajabu kuona mandhari maridadi

Mungu Ni Nani?

Watu wengi husema kwamba wanamwamini Mungu. Lakini ukiwauliza Mungu ni nani, utapata majibu tofauti-tofauti. Baadhi yao humwona Mungu kuwa hakimu mkatili ambaye lengo lake ni kuwaadhibu tu watu wanaokosea. Wengine nao hufikiri kwamba, hata wafanye nini, sikuzote Mungu ni mwenye upendo na yuko tayari kuwasamehe. Ilhali wengine wanaamini kwamba Mungu yuko mbali sana na hajali hali yetu ikoje. Kwa kuwa maoni kumhusu Mungu yanatofautiana sana, huenda watu wengi wakahisi kwamba haiwezekani kabisa kumjua.

Je, ni muhimu kumjua Mungu? Ndiyo. Kumjua Mungu vizuri kutafanya maisha yako yawe na kusudi. (Matendo 17:26-28) Kadiri unavyomkaribia, ndivyo atakavyokupenda zaidi na kukusaidia pia. (Yakobo 4:8) Isitoshe, kuwa na ujuzi sahihi kumhusu Mungu kutakuwezesha uishi milele.—Yohana 17:3.

Unaweza kufanya nini ili umjue Mungu? Hebu fikiria kuhusu mtu unayemfahamu vizuri, kama vile rafiki yako wa karibu. Urafiki wenu ulianzaje? Inaelekea ulianza kwa kujua jina lake, sifa zake, mambo anayopenda na asiyopenda, mambo ambayo amefanya na anayopanga kufanya, na kadhalika. Kwa hiyo, ulisitawisha urafiki naye baada ya kujua mambo mbalimbali kumhusu.

Vivyo hivyo, ili tumjue Mungu, tunahitaji kujua mambo yafuatayo kumhusu:

  • ANAITWA NANI?

  • ANA SIFA GANI?

  • AMEFANYA MAMBO GANI?

  • ATAFANYA NINI WAKATI UJAO?

  • UTANUFAIKAJE KWA KUMJUA?

Gazeti hili linafafanua majibu ambayo Biblia inatoa kuhusu maswali hayo. Litakusaidia kumjua Mungu na pia utajifunza faida za kusitawisha uhusiano wa karibu na yeye.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki