Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp20 Na. 2 kur. 4-5
  • Kwa Nini Tunahitaji Ufalme wa Mungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Tunahitaji Ufalme wa Mungu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MWANZO WA UTAWALA WA WANADAMU
  • MUDA WA KUCHUKUA HATUA UMEKARIBIA!
  • Ufalme wa Mungu—Utawala Mpya wa Dunia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Muda Ambao Mungu Ameruhusu Kuteseka Wakaribia Kwisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Suala Linalokuhusu Wewe
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Utawala wa Yehova Umethibitika Kuwa Bora!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
wp20 Na. 2 kur. 4-5
Adamu na Hawa wakiangalia maporomoko ya maji katika bustani ya Edeni.

Mungu alipotawala, viumbe wote waliishi kwa amani na umoja

Kwa Nini Tunahitaji Ufalme wa Mungu?

Mwanzoni mwa historia ya wanadamu, Muumba wetu, ambaye jina lake ni Yehova, ndiye alikuwa Mtawala pekee. Alitawala kwa upendo. Aliwatayarishia wanadamu makao maridadi ya kuishi, yaani, bustani ya Edeni. Pia, aliwapatia chakula kingi. Isitoshe, Yehova aliwapatia wanadamu kazi nzuri sana. (Mwanzo 1:28, 29; 2:8, 15) Wanadamu wangeendelea kufurahia amani ikiwa wangemruhusu Mungu aendelee kuwatawala kwa upendo.

Adamu akiwa ameshika tunda lililokatazwa ambalo amepewa na Hawa.

Wanadamu wa kwanza walimkataa Mungu kuwa Mtawala wao

Biblia inaonyesha kwamba malaika mwasi, ambaye baadaye aliitwa Shetani Ibilisi, alitilia shaka haki ya Mungu ya kutawala. Alidai kwamba wanadamu watakuwa na furaha wakikataa kutawaliwa na Mungu na wakiacha kufuata mwongozo wake. Kwa kusikitisha, wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Hawa, walimsikiliza Shetani nao wakamwasi Mungu.—Mwanzo 3:1-6; Ufunuo 12:9.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walimkataa Mungu kuwa Mtawala wao, walifukuzwa kutoka katika Paradiso na kupoteza tumaini la kuishi milele wakiwa na afya kamilifu. (Mwanzo 3:17-19) Uamuzi wao uliathiri watoto wao wote. Biblia inasema kwamba kwa sababu ya dhambi ambayo Adamu alifanya, “dhambi iliingia katika ulimwengu na kifo kupitia dhambi.” (Waroma 5:12) Dhambi ilikuwa na matokeo mengine mabaya: “Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwenzake kwa kumuumiza.” (Mhubiri 8:9) Hilo linamaanisha kwamba wanadamu wanapojitawala, lazima matatizo yatokee.

MWANZO WA UTAWALA WA WANADAMU

Nimrodi akiwa amesimama kwa kiburi. Nyuma yake kuna watu wanaojenga.

Nimrodi alimwasi Yehova

Mtawala wa kwanza wa wanadamu anayetajwa katika Biblia aliitwa Nimrodi. Aliasi utawala wa Yehova. Tangu siku za Nimrodi, watu wenye mamlaka wametumia mamlaka yao vibaya kuwaumiza wengine. Miaka 3,000 hivi iliyopita, Mfalme Sulemani aliandika hivi: “Nikaona machozi ya wanaokandamizwa, na hakukuwa na mtu yeyote wa kuwafariji. Na wale waliowakandamiza walikuwa na nguvu.”—Mhubiri 4:1.

Mambo hayajabadilika leo. Mwaka 2009, chapisho moja la Umoja wa Mataifa lilisema kwamba utawala mbaya umeonekana kuwa chanzo cha mambo maovu yanayoendelea duniani leo.

MUDA WA KUCHUKUA HATUA UMEKARIBIA!

Ulimwengu unahitaji watawala bora na utawala mzuri. Muumba wetu ametuahidi jambo hilo!

Mkusanyo wa picha: Matokeo ya utawala wa wanadamu. 1. Mwanamke wa Asia ameketi kwenye mazingira machafu akiwa amembeba mtoto wake anayelia. 2. Mwanamume mzee amelazwa hospitalini. 3. Wanajeshi wakifyatua risasi vitani. 4. Waandamanaji wenye hasira wakipiga kelele na kuinua mabango. 5. Mwanamke na binti yake wamesimama nje ya mlango wa nyumba yao uliovunjwa. 6. Jiji limetanda moshi na waya za umeme.

Hata serikali bora za wanadamu zimeshindwa kusuluhisha matatizo makubwa ya wanadamu

Mungu ameusimamisha Ufalme au utawala ambao utaondoa serikali zote za wanadamu, “nao pekee utasimama milele.” (Danieli 2:44) Huo ndio Ufalme ambao mamilioni ya watu wamekuwa wakiomba uje. (Mathayo 6:9, 10) Lakini Mungu amemchagua mtawala wa serikali Yake. Mtawala huyo amewahi kuwa mwanadamu. Mungu amemchagua nani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki