Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb19 Juni uku. 7
  • Chagua Burudani kwa Hekima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chagua Burudani kwa Hekima
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Chagua Burudani Inayomfurahisha Yehova
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Jinsi ya Kuchagua Burudani
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
  • Jinsi ya Kuchagua Burudani Inayofaa
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
  • Waweza Kupata Vitumbuizo Vifaavyo
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
mwb19 Juni uku. 7

MAISHA YA MKRISTO

Chagua Burudani kwa Hekima

Kwa nini tunapaswa kuchagua burudani kwa hekima? Kwa sababu tunapochagua sinema ya kutazama, wimbo wa kusikiliza, tovuti ya kutembelea, kitabu cha kusoma, au mchezo wa video tutakaocheza, tunaamua jambo tunalotaka kujaza katika akili yetu. Mambo tunayochagua huathiri tabia yetu. Kwa kusikitisha, burudani nyingi zinazopatikana leo zinahusisha mambo ambayo Yehova anashutumu. (Zb 11:5; Gal 5:19-21) Kwa sababu hiyo, Biblia inatusihi tuendelee kufikiria mambo ambayo yanamtukuza Yehova.—Flp 4:8.

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA NICHAGUE BURUDANI YA AINA GANI? KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Mchezo wa wapiganaji wa kale wa Roma

    Michezo ya wapiganaji wa kale wa Roma ina ulinganifu gani na burudani fulani za leo?

  • Ndugu ambaye ni painia akihubiri pamoja na kijana kutanikoni

    Washiriki wa kutaniko wanaweza kuwasaidiaje vijana kuchagua burudani kwa hekima?

  • Askari

    Waroma 12:9 inapaswa kutusaidiaje tunapochagua burudani?

  • Mashahidi vijana wakicheza mpira

    Ni mifano gani ya burudani inayofaa katika eneo lenu?

BURUDANI YAKO INAKUFANYA UTENDE AU UKETI TU?

Siku hizi, burudani ambayo watu wengi wanapenda inawazoeza kuketi tu badala ya kuwa watendaji. Sinema, vitabu, na vipindi vya televisheni huonyesha ubunifu wa mtu mwingine, si wako. Ingawa kuna mahali pa burudani isiyohusisha utendaji wako binafsi, wengi wameona kwamba inathawabisha zaidi ikiwa wewe unahusika zaidi. Kwa mfano, watu fulani hufurahia kupiga kifaa cha muziki au kuchora picha. Wengine hufurahia tafrija zinazofanywa nje zinazomfanya mhusika atende kama vile kucheza mchezo fulani au kwenda matembezi au kuogelea. Hata iwe tutachagua burudani gani, acheni “[tufanye] mambo yote kwa utukufu wa Mungu.”—1Ko 10:31.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki