Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb14 uku. 168
  • Nimeazimia Kumtumikia Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nimeazimia Kumtumikia Yehova
  • 2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Habari Zinazolingana
  • Ninaipenda Sana Nchi ya Sierra Leone
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Kazi ya Kufanya Wanafunzi Imefinyanga Maisha Yangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Kitu Bora Zaidi Kuliko Almasi
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Tuliwakimbia Wanajeshi Waasi
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
Pata Habari Zaidi
2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
yb14 uku. 168

SIERRA LEONE NA GUINEA

Nimeazimia Kumtumikia Yehova

Philip Tengbeh

  • ALIZALIWA 1966

  • ALIBATIZWA 1997

  • MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Mkimbizi ambaye alisaidia kujenga Majumba matano ya Ufalme.

Picha katika ukurasa wa 168

MNAMO 1991, mimi na mke wangu, Satta, tulikimbia ili kuokoa maisha yetu wakati wanajeshi waasi walipouvamia mji tulioishi, Koindu, nchini Sierra Leone. Kwa zaidi ya miaka nane, tuliishi katika kambi mbalimbali za wakimbizi. Katika kambi hizo, tulikabiliana na hali ngumu kama vile upungufu wa chakula, magonjwa na tulizungukwa na majirani waliojihusisha katika upotovu wa maadili.

Katika kila kambi, tuliziomba kiwanja mamlaka husika ili tujenge Jumba la Ufalme. Nyakati fulani maombi yetu yalikubaliwa au kukataliwa. Hata hivyo, siku zote tulipanga mahali pa kukutana kwa ajili ya ibada. Tulikuwa tumeazimia kumtumikia Yehova. Hatimaye, tulijenga Majumba ya Ufalme manne katika kambi hizo.

Vita vilipoisha, hatungeweza kurudi nyumbani. Mji wa Koindu ulikuwa umeharibiwa kabisa na mapigano hayo yaliyodumu kwa miaka kadhaa. Kwa hiyo tukapelekwa kwenye kambi nyingine ya wakimbizi iliyokuwa karibu na jiji la Bo. Tukiwa huko, ofisi ya tawi ilitoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa Jumba la Ufalme, hivyo tukajenga jumba la tano.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki