Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 171
  • Ibilisi Ana Mwonekano Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ibilisi Ana Mwonekano Gani?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jibu la Biblia
  • Biblia inamfafanuaje Ibilisi?
  • Mpinge Shetani, Naye Atakimbia!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • ‘Mpinge Ibilisi’ Kama Yesu Alivyofanya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Adui wa Uzima wa Milele
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Majibu ya Maswali ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 171

Ibilisi Ana Mwonekano Gani?

Jibu la Biblia

Ibilisi ni kiumbe wa roho asiyeonekana, hilo linamaanisha hana mwili wa nyama ambao tunaweza kuuona.—Waefeso 6:11, 12.

Wasanii wengi wamemchora Ibilisi akiwa ameshika mti mrefu wenye meno. Anafanana na mbuzi mwenye pembe na mkia.

Wasanii wengi wamemchora Ibilisi kama kiumbe anayefanana na mbuzi mwenye pembe na mkia, na ameshika mti mrefu wenye meno. Baadhi ya watu wamesema kwamba michoro hiyo ilichorwa miaka 1000 hivi iliyopita na watu ambao huenda waliathiriwa na hadithi na hekaya za kale.

  • Biblia inamfafanuaje Ibilisi?

  • Mistari ya Biblia kumhusu Ibilisi

Biblia inamfafanuaje Ibilisi?

Biblia inatumia njia kadhaa kumfafanua Ibilisi. Mifano hiyo inatusaidia kuelewa utu wake, si mwonekano wake. Baadhi ya mifano hiyo ni:

  • Malaika wa nuru. Anajaribu kufanya watu wafuate mafundisho yake badala ya mafundisho ya Mungu kwa kujifanya anawapa kitu bora.—2 Wakorintho 11:14.

  • Simba anayenguruma. Anawashambulia vikali waabudu wa Mungu.—1 Petro 5:8.

  • Joka mkubwa. Anatisha, ni mwenye nguvu, na husababisha uharibifu.—Ufunuo 12:9.

Mistari ya Biblia kumhusu Ibilisi

  • 2 Wakorintho 11:14: “Shetani mwenyewe huendelea kujifanya kuwa malaika wa nuru.”

    Maana: Shetani anajifanya kuwa mwema ili awadanganye watu wafuate mafundisho yake badala ya mafundisho ya Mungu.

  • Waefeso 6:11: “Vaeni mavazi kamili ya silaha kutoka kwa Mungu ili mweze kusimama imara dhidi ya matendo yenye hila ya Ibilisi.”

    Maana: Shetani hupanga njama zenye uovu ili kuwafanya watu wasimtii Mungu.

  • Yakobo 4:7: “Jitiisheni kwa Mungu; lakini mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia ninyi.”

    Maana: Mtu anaweza kumshinda Ibilisi kwa kumtii Mungu badala ya Ibilisi.

  • 1 Petro 5:8: “Adui yenu, Ibilisi, anatembea huku na huku kama simba anayenguruma, akitafuta kummeza mtu.”

    Maana: Ibilisi huwachukia wale wanaomtii Mungu na hutaka kuharibu urafiki wao pamoja na Mungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki