Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 172
  • Maria Magdalene Alikuwa Nani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maria Magdalene Alikuwa Nani?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jibu la Biblia
  • Je, Maria Magdalene alikuwa kahaba?
  • Je, Maria Magdalene alikuwa “mtume wa mitume”?
  • Je, Maria Magdalene alikuwa mke wa Yesu Kristo?
  • “Nimemwona Bwana!”
    Igeni Imani Yao
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Mfano wa Maria Unatufundisha Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 172
Maria Magdalene akimwona Yesu nje ya kaburi lake baada ya kufufuliwa.

Maria Magdalene Alikuwa Nani?

Jibu la Biblia

Maria Magdalene alikuwa mfuasi mwaminifu wa Yesu Kristo. Inaelekea jina lake, Magdalene, lilitokana na mji wa Magdala (huenda Magadan), ambalo lilikuwa karibu na Bahari ya Galilaya. Huenda Maria aliwahi kuishi katika eneo hilo.

Maria Magdalene alikuwa mmoja kati ya wanawake waliosafiri pamoja na Yesu na wanafunzi wake na kuwategemeza kimwili. (Luka 8:1-3) Alishuhudia Yesu alipokuwa anauawa, na alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumwona Yesu baada ya kufufuliwa.—Marko 15:40; Yohana 20:11-18.

  • Je, Maria Magdalene alikuwa kahaba?

  • Je, Maria Magdalene alikuwa “mtume wa mitume”?

  • Je, Maria Magdalene alikuwa mke wa Yesu Kristo?

  • Kuna Maria wangapi wanaotajwa katika Biblia?

Je, Maria Magdalene alikuwa kahaba?

Biblia haisemi kwamba Maria Magdalene alikuwa kahaba. Biblia inataja tu kwamba Yesu alitoa roho waovu saba ndani ya Maria.—Luka 8:2.

Wazo la kwamba alikuwa kahaba lilitoka wapi? Miaka mingi baada ya kifo chake, watu walidai kwamba alikuwa yule mwanamke ambaye alilowesha miguu ya Yesu kwa machozi na kuifuta kwa nywele za kichwa chake. (Luka 7:36-38) Hata hivyo, hakuna sehemu yoyote katika Biblia inayounga mkono jambo hilo.

Je, Maria Magdalene alikuwa “mtume wa mitume”?

Hapana. Kanisa Katoliki linamwita Maria “Mt. Maria Magdalene” na pia “mtume aliyetumwa kwa mitume” kwa sababu alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwajulisha wanafunzi kwamba Yesu amefufuliwa. (Yohana 20:18) Lakini jambo hilo halimaanishi kwamba alikuwa mtume. Na hakuna mahali ambapo Maandiko yanamwita hivyo.—Luka 6:12-16.

Biblia ilikamilika mwishoni mwa karne ya kwanza W.K. Hata hivyo, mpaka karne ya sita ndipo wenye mamlaka katika kanisa walipofanya uamuzi wa kumpandisha cheo. Maandishi yaliyoandikwa katika karne ya pili na ya tatu—ambayo si sehemu ya Biblia—yanasema kwamba baadhi ya mitume wa Yesu walimwonea wivu Maria. Habari kama hizo zilizotungwa hazina msingi wowote wa Kimaandiko.

Je, Maria Magdalene alikuwa mke wa Yesu Kristo?

Hapana. Biblia inataja moja kwa moja kwamba Yesu alikuwa mseja.a

a Ona makala yenye kichwa “Je, Yesu Alikuwa na Mke? Je, Alikuwa na Ndugu na Dada?”

Kuna Maria wangapi wanaotajwa katika Biblia?

Biblia inataja wanawake sita wanaoitwa Maria.b

  1. 1. Mama ya Yesu.—Mathayo 1:18.

  2. 2. Dada ya Martha na Lazaro.—Yohana 11:1, 2.

  3. 3. Maria Magdalene.—Luka 8:2.

  4. 4. Mama ya Yakobo na Yose.—Mathayo 27:56.

  5. 5. Mama ya Yohana Marko.—Matendo 12:12.

  6. 6. Mkristo aliyekuwa Roma ambaye alifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kutaniko la huko.—Waroma 16:6.

b Maria ni jina la Kigiriki linalotokana na jina la Kiebrania Miriamu, ambalo lilikuwa pia jina la dada ya Musa.—1 Mambo ya Nyakati 6:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki