Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwyp makala 108
  • Umaarufu Mtandaoni Ni Muhimu Kadiri Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umaarufu Mtandaoni Ni Muhimu Kadiri Gani?
  • Vijana Huuliza
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna hatari zipi?
  • “Ndoto ya umaarufu”
  • Wafuasi na alama ya kupenda ni muhimu kadiri gani?
  • Kuna Ubaya Kufanya Urafiki Kupitia Intaneti?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Je, Ni Vibaya Kuwa Maarufu?
    Amkeni!—2012
  • Jinsi ya Kuwasaidia Vijana Waepuke Hatari Kwenye Intaneti
    Amkeni!—2014
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Vituo vya Mawasiliano?—Sehemu ya 2
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Vijana Huuliza
ijwyp makala 108
Msichana akitabasamu huku akitazama simu yake ya mkononi. Amepokea alama 85 za kupenda kitu alichoweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

VIJANA HUULIZA

Umaarufu Mtandaoni Ni Muhimu Kadiri Gani?

Msichana fulani anayeitwa Elaine anasema hivi: “Nilipoona kwamba wanafunzi wenzangu walikuwa na mamia ya watu wanaowafuata kwenye mitandao ya kijamii, nilijiambia, ‘Kwa kweli, wao ni maarufu!’ Lazima nikiri kwamba niliwaonea wivu kidogo.”

Je, umewahi kuhisi hivyo? Ikiwa ndivyo, makala hii itakusaidia kuepuka mahangaiko ya kujaribu kuwa maarufu kwenye Intaneti.

  • Kuna hatari zipi?

  • “Ndoto ya umaarufu”

  • Wafuasi na alama ya kupenda ni muhimu kadiri gani?

  • Jihadhari na “unyenyekevu wa kinafiki”

Kuna hatari zipi?

Kwenye Methali 22:1, Biblia inasema kwamba “afadhali kuchagua jina jema kuliko mali nyingi.” Kwa hiyo, hakuna ubaya kutaka kuwa na sifa nzuri, au kutaka kupendwa.

Lakini nyakati fulani tamaa ya kukubaliwa inaweza kubadilika kuwa tamaa ya kupata umaarufu. Je, kuna hatari ya kufanya hivyo? Onya, mwenye umri wa miaka 16, anaweza kusema ndiyo:

“Nimewaona watu wakifanya mambo ya ajabu, kama vile kuruka kutoka kwenye orofa ya pili shuleni, ili tu wapate umaarufu.”

Watu fulani hurekodi video ya mambo ya kipumbavu wanayofanya na kuiweka kwenye mtandao ili tu wengine wawatambue. Kwa mfano, baadhi ya vijana waliweka video kwenye mtandao iliyowaonyesha wakila sabuni zenye sumu, jambo ambalo hakuna mtu anayepaswa kamwe kufanya!

Biblia inasema hivi: “Msifanye chochote . . . kwa majivuno ya bure.”—Wafilipi 2:3, Biblia Habari Njema.

Jambo la kufikiria:

  • Kupata umaarufu kwenye mtandao ni muhimu kadiri gani kwako?

  • Je, unaweza kuhatarisha afya au uhai wako ili tu rafiki zako wakutambue au wakukubali?

    Vijana wenzako wanasema nini

    Leianna.

    “Umaarufu ni hatari watu wanapoanza kuwa na mtazamo wa kufanya chochote kile, na kufikiri kwamba wakizungumza, kuvaa, au kutenda kwa njia fulani​—hata mtandaoni​—watakuwa maarufu. Si jambo la hekima kukiuka imani na kanuni zako ili tu kupata umaarufu.”​—Leianna.

“Ndoto ya umaarufu”

Si nyakati zote ambazo watu hufanya mambo hatari ili kujipatia umaarufu. Erica, mwenye umri wa miaka 22, anaeleza jinsi watu fulani hutumia mbinu nyingine:

“Watu fulani huweka picha nyingi sana za maisha yao, ili kufanya ionekane kwamba wana marafiki wengi sana wa karibu ambao wanatumia wakati pamoja nao. Hilo huwafanya wengine wafikiri wao ni maarufu sana.”

Cara, mwenye umri wa miaka 15, anasema kwamba watu fulani hutumia uwongo ili kufanya ionekane wao ni maarufu:

“Nimewahi kuwaona watu wakipachika picha za uwongo ili tu waonekane kwamba walikuwa kwenye karamu fulani wakati kwa kweli walikuwa nyumbani.”

Matthew, mwenye umri wa miaka 21, anakiri kwamba amewahi kufanya jambo kama hilo:

“Niliweka picha fulani na kusema nilikuwa nimepanda juu ya Mlima Everest, ingawa sijawahi kwenda Asia hata mara moja!”

Biblia inasema hivi: “Tunataka kujiendesha kwa unyoofu katika mambo yote.”—Waebrania 13:18.

Jambo la kufikiria:

  • Unapotumia mitandao ya kijamii, je, wewe hutumia uwongo ili tu uwe maarufu?

  • Je, picha na maelezo unayoweka yanaonyesha jinsi ulivyo kikweli na viwango vyako?

    Vijana wenzako wanasema nini

    Hannah.

    “Watu fulani watafanya chochote kile ili tu wapate alama za kupendwa. Lakini je, ungependa kujulikana kwa sababu ya kuzungumza na kuvalia kwa njia isiyofaa na pia kwa kujionyesha unamiliki vitu gani? Au ungependa kujulikana kwa sifa zako nzuri au kwamba unapendezwa kikweli na wengine? Kupendwa kunakufanya ujihisi vizuri, lakini hakikisha unapendwa kwa sababu nzuri?”​—Hannah.

Wafuasi na alama ya kupenda ni muhimu kadiri gani?

Watu wengi huamini kwamba umaarufu kwenye mtandao unategemea kuwa na wafuasi wengi na alama nyingi za watu kupenda walichopachika. Matthew, aliyenukuliwa awali, anakiri kwamba zamani alihisi hivyo:

“Ningewauliza watu, ‘Wewe una wafuasi wangapi?’ au ‘Ni kiasi gani cha juu zaidi ambacho umewahi kupata za alama ya kupendwa?’ Ili kuongeza idadi ya wafuasi, ningewafuata watu ambao hata sikuwajua, nikitarajia kwamba wangenifuata pia. Nilisitawisha pupa ya kupata umaarufu, na mtandao wa kijamii ulichochea pupa hiyo.”

Picha: 1. Msichana akitabasamu huku akitazama simu yake ya mkononi. 2. Msichana huyohuyo akila bakuli iliyojaa vyakula visivyo na lishe. 3. Msichana huyo akiwa ameshika tumbo huku akijihisi mgonjwa.

Umaarufu mtandaoni ni kama chakula kisicho na lishe—huenda kikafaa kwa muda mfupi lakini hakitoshelezi mahitaji yako

Maria, mwenye umri wa miaka 25, anasema kwamba watu fulani hupima thamani yao kwa idadi ya wafuasi na alama za kupendwa wanazopokea:

“Msichana anapoweka picha yake na isipate alama nyingi kwamba watu wanaipenda, atakata kauli kwamba yeye si mrembo. Bila shaka, huo ni uamuzi usiofaa, lakini watu wengi katika hali hiyo wangeitikia kama yeye. Ni kana kwamba wanajinyanyasa kwenye mtandao.”

Biblia inasema hivi: “Tusiwe tukijisifu, tusichochee mashindano kati yetu, wala tusioneane wivu.”—Wagalatia 5:26.

Jambo la kufikiria:

  • Ikiwa unatumia mitandao ya kijamii, je, wewe huona inakuchochea ujilinganishe na wengine?

  • Je, wewe huona idadi ya wafuasi kuwa muhimu kuliko kuwa na marafiki wanaokujali kikweli?

    Vijana wenzako wanasema nini

    Joshua.

    “Ili uwe maarufu mtandaoni lazima uwe mtu ambaye watu wanataka kuiga, na kwa kawaida watu hutaka kuiga wale ambao wana sifa wanazopenda. Hilo linaweza kukufanya ukazie fikira sana jinsi wengine wanavyokuona na jinsi unavyoweza kuwapendeza. Ni jambo la kawaida kutaka kupendwa, lakini kukazia fikira kuwa maarufu kunaweza kufanya tamaa hiyo iwe jambo kuu maishani mwako.”​—Joshua.

Jihadhari na “unyenyekevu wa kinafiki”

Je, umewahi kuona watu wakijifanya wanalalamika lakini kwa kweli wanajisifu kuhusu mambo waliyotimiza?

  • “Tangu niliponunua gari jipya, watu wanashinda wakiniomba lifti!”

  • “Sipendi jinsi kila mtu anavyonipongeza kwa kupunguza uzito!”

Anayezungumza analalamika ili ionekane yeye ni mnyenyekevu—ingawa kwa kweli anajisifu.

Onyo: Mbinu hii ya kujisifu haifanikiwi, kwa sababu wengine hutambua unachojaribu kufanya. Na kwa kuwa unyenyekevu huo ni wa kinafiki, watu huuchukia zaidi kuliko kujisifu waziwazi.

Wakati ujao unapoweka ujumbe au picha kwenye mtandao wa kijamii, jihadhari kuhusu unyenyekevu wa kinafiki. Fuata ushauri huu wenye hekima wa Biblia: “Acha mtu mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe.”—Methali 27:2.

Muhtasari: Umaarufu Mtandaoni Ni Muhimu Kadiri Gani?

  • Hakikisha chochote unachoweka mtandaoni kinaonyesha jinsi ulivyo kikweli na viwango vyako.

  • Uwe mnyoofu kuhusu mambo unayoweka mtandaoni.

  • Uwe na maoni yaliyosawazika kuhusu wafuasi na alama ya kupendwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki