Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwhf makala 4
  • Kuzungumza na Watoto Kuhusu Kileo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuzungumza na Watoto Kuhusu Kileo
  • Msaada kwa Ajili ya Familia
  • Habari Zinazolingana
  • Kutumia Kileo Vibaya—Kunaathiri Afya
    Amkeni!—2005
  • Dumisha Maoni Yaliyosawazika Kuhusu Kutumia Kileo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Fuata Mwongozo wa Mungu Kuhusu Kileo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Mtazamo Unaofaa Kuhusu Pombe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Msaada kwa Ajili ya Familia
ijwhf makala 4
Msichana mdogo anawatazama wazazi wake wakinywa kileo

MSAADA KWA AJILI YA FAMILIA

Kuzungumza na Watoto Kuhusu Kileo

“Mara ya kwanza tulipozungumza na binti yetu kuhusu kileo, alikuwa na umri wa miaka sita. Tulishangaa kugundua kwamba alijua mengi kuliko tulivyotarajia.”​—Alexander.

  • Unachopaswa kujua

  • Unachoweza kufanya

  • Biblia inasema nini kuhusu kileo?

Unachopaswa kujua

Kuzungumza na watoto kuhusu kileo ni muhimu. Usingoje hadi mtoto wako afikie umri wa utineja. Khamit anayeishi Urusi anasema hivi: “Afadhali tungalizungumza mapema na mwana wetu kuhusu matumizi yanayofaa ya kileo. Nilitambua umuhimu wa kufanya hivyo ilipokuwa kuchelewa mno. Niligundua kwamba mwanangu alikuwa akinywa kwa ukawaida alipokuwa na umri wa miaka 13.”

Kwa nini jambo hilo likuhangaishe?

  • Mtoto wako anaweza kuathiriwa na wanafunzi wenzake, matangazo ya biashara, na Televisheni, na hivyo kuwa na maoni yasiyofaa kuhusu kileo.

  • Kulingana na Vituo vya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza vya Marekani, asilimia 11 ya watu wanaokunywa kileo nchini Marekani ni vijana ambao hawajafikisha umri unaoruhusiwa na sheria.

Haishangazi kwamba maofisa wa afya wanapendekeza wazazi wawaelimishe watoto wao tangu wanapokuwa wachanga kuhusu hatari za kileo. Unawezaje kufanya hivyo?

Unachoweza kufanya

Fikiria mapema maswali ambayo mtoto wako anaweza kuuliza. Watoto ni wadadisi, na watoto wakubwa ni wadadisi hata zaidi. Hivyo, ni vema utayarishe jinsi utakavyojibu. Kwa mfano:

  • Ikiwa mtoto wako angependa kujua ladha ya kileo, unaweza kumwambia kwamba divai ni kama maji ya matunda yenye uchachu na bia ni chungu.

  • Ikiwa mtoto wako anataka kuonja kileo, unaweza kumwambia miili ya watoto haiwezi kuhimili kileo. Taja matokeo ya kunywa: Kileo kinaweza kumfanya mtu ahisi ametulia, lakini akinywa sana anaweza kuhisi kizunguzungu, kutenda kipumbavu, au kusema na kufanya mambo ambayo atajutia.​—Methali 23:29-​35.

Jielimishe. Biblia inasema hivi: “Mtu mwerevu hutenda kwa ujuzi.” (Methali 13:16) Tafuta habari kuhusu matumizi ya kileo, sheria, na viwango vinavyoruhusiwa katika nchi yenu. Utakuwa umejiandaa vizuri kumsaidia mtoto wako.

Chukua hatua ya kwanza kuzungumzia jambo hilo. Mark, ambaye ni baba nchini Uingereza anasema: “Watoto wanaweza kuchanganyikiwa wanapofikiria suala la kileo. Nilimuuliza mwana wangu mwenye umri wa miaka minane ikiwa alifikiri ni sawa au si sawa kunywa kileo. Niliandaa mazingira matulivu, na hilo lilimsaidia kueleza maoni yake waziwazi.”

Utamsaidia zaidi ukizungumzia suala hilo mara kadhaa. Ikitegemea umri wa mtoto tia ndani mazungumzo kuhusu kileo pamoja na masuala mengine maishani, kama usalama barabarani na elimu ya ngono.

Weka kielelezo kinachofaa. Watoto ni kama sifongo, wanafyonza kila kitu kwenye mazingira, na utafiti unaonyesha kwamba wazazi ndio walio na uvutano mkubwa zaidi kwa watoto wao. Hiyo inamaanisha kwamba ikiwa kileo ndiyo njia yako ya msingi ya kutulia au kupunguza mkazo, mtoto wako ataelewa kwamba kileo ndiyo njia ya kuondoa mahangaiko maishani. Basi weka mfano mzuri wa kuigwa. Hakikisha kwamba unatumia kileo kwa hekima.

Msichana akimwona mama akikataa kuongezwa divai

Watoto wako watajifunza kuhusu kileo kutokana na mfano wako

Biblia inasema nini kuhusu kileo?

Yehova ametokeza “divai inayofanya moyo wa mwanadamu ushangilie.” (Zaburi 104:14, 15) Kileo si kiovu; ni zawadi kutoka kwa Mungu.

“Divai ni mdhihaki, kileo ni vurugu; yeyote anayepotoshwa navyo hana hekima.” (Methali 20:1) Kileo kinapaswa kutumiwa kwa hekima.

“Walevi . . . hawataurithi Ufalme wa Mungu.” (1 Wakorintho 6:​10) Mungu anashutumu matumizi mabaya ya kileo, si kutumia kileo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki