Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwwd makala 13
  • Ngozi ya Tunda la Balungi Inayoweza Kuhimili Mshtuko

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ngozi ya Tunda la Balungi Inayoweza Kuhimili Mshtuko
  • Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Habari Zinazolingana
  • Linda Ngozi Yako!
    Amkeni!—2005
  • Ngozi ya nyoka
    Amkeni!—2014
  • Ngozi Yako Ni Kama “Ukuta wa Jiji”
    Amkeni!—2004
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Je, Ni Kazi ya Ubuni?
ijwwd makala 13
Tunda la Balungi likiwa limening’inia mtini.

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Ngozi ya Tunda la Balungi Inayoweza Kuhimili Mshtuko

Balungi ni tunda kubwa tamu la jamii ya chungwa linalokua kwenye mti. Tunda hilo halibondeki hata baada ya kuanguka mita 10 kutoka juu kwenye mti! Ni nini kinachofanya tunda hilo liwe na uwezo wa kuhimili mshtuko wa namna hiyo?

Jambo la Kufikiria: Watafiti wamegundua kwamba sehemu nyeupe iliyo ndani ya ganda la Balungi ina chembe zenye nafasi kama za sponji. Nafasi hizo huzidi kuwa pana kuelekea ndani ya tunda, nazo zimejaa hewa au umajimaji. Kwa hiyo, tunda hilo linapoanguka chini, umajimaji huo unakuwa kama mto. Ngozi ya tunda la Balungi inasinyaa na kuwa ngumu, na kuwa imara badala ya kupasuka.

Tunda la Balungi lililokatwa ili kuona unene wa ngozi yake. Picha ndogo iliyokuzwa inaonyesha nafasi zilizo ndani ya ganda.

Wanasayansi wanajaribu kubuni aina fulani ya chuma ambayo itaweza kuhimili mshtuko kama ngozi ya tunda la Balungi. Wanaamini kwamba kitu kama hicho kinaweza kutumika pia katika kubuni kofia za wanaoendesha pikipiki, vifaa vya kulinda magari wakati wa aksidenti, na vifaa vya kulinda vituo vya angani dhidi ya vimondo.

Una maoni gani? Je, ngozi ya tunda la Balungi ilijitokeza yenyewe? Au ilibuniwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki