27 Baada ya mwanamke huyo kunyweshwa maji hayo, ikiwa amejichafua na kukosa uaminifu kwa mume wake, maji yanayoleta laana yataingia mwilini mwake na kusababisha maumivu makali, na tumbo lake litavimba naye atakuwa tasa, na mwanamke huyo atakuwa mfano wa laana miongoni mwa watu wake.