12 Basi Delila akachukua kamba mpya akamfunga nazo, kisha akamwambia hivi Samsoni kwa sauti kubwa: “Wafilisti wamekuja kukushambulia, Samsoni!” (Wakati huo watu waliokuwa wakimvizia walikuwa wamejificha katika chumba cha ndani.) Ndipo akazikata kamba hizo kutoka mikononi mwake kama nyuzi.+