2 Watu wa kabila la Dani wakawatuma wanaume watano mashujaa kutoka miongoni mwao, waliotoka Sora na Eshtaoli,+ ili waipeleleze nchi na kuichunguza. Wakawaambia, “Nendeni mkaichunguze nchi.” Walipofika kwenye eneo lenye milima la Efraimu, nyumbani kwa Mika,+ wakalala huko usiku huo.