9 Yule mwanamume alipotaka kuondoka pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani, baba ya yule msichana, akamwambia, “Tazama! Mchana umekwisha, jioni inakaribia. Tafadhali, lala hapa usiku huu, ustarehe. Amkeni mapema kesho na kuanza safari yenu ya kwenda nyumbani kwenu.”