4 Walipoamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Yehova. Kichwa cha Dagoni na vitanga vya mikono yake miwili vilikuwa vimekatwa, navyo vilikuwa chini kwenye kizingiti. Ni sehemu tu yenye umbo la samaki ndiyo iliyobaki.