3 Kutoka huko nenda mpaka kwenye mti mkubwa wa Tabori, na huko utakutana na wanaume watatu wakipanda kwenda kwa Mungu wa kweli kule Betheli,+ mmoja akiwa amebeba wanambuzi watatu, mwingine akiwa amebeba mikate mitatu, na mwingine akiwa amebeba mtungi mkubwa wa divai.