7 Kwa hiyo akachukua ng’ombe dume wawili, akawakata vipandevipande, akawatuma wajumbe wavipeleke katika eneo lote la Israeli wakisema: “Mtu yeyote ambaye hamfuati Sauli na Samweli ajue kwamba ng’ombe wake watafanyiwa hivi!” Na watu wakashikwa na hofu ya Yehova hivi kwamba wakatoka wote pamoja.