8 Ninyi nyote mmepanga njama dhidi yangu! Hakuna yeyote aliyenijulisha wakati mwana wangu mwenyewe alipofanya agano na mwana wa Yese!+ Hakuna yeyote kati yenu anayenihurumia na kunijulisha kwamba mwanangu mwenyewe amemchochea mtumishi wangu mwenyewe dhidi yangu ili anivizie, kama hali ilivyo sasa.”