17 Ndipo mfalme akawaambia walinzi waliomzunguka: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Yehova, kwa sababu wamemuunga mkono Daudi! Walijua kwamba ametoroka, lakini hawakunijulisha!” Lakini watumishi hao wa mfalme hawakutaka kuinua mikono yao wawashambulie makuhani wa Yehova.