3 Lakini wakuu wa Wafilisti wakauliza: “Waebrania hawa wamekuja kufanya nini?” Akishi akawajibu hivi wakuu wa Wafilisti: “Huyu ni Daudi, mtumishi wa Mfalme Sauli wa Israeli, naye ameishi pamoja nami kwa mwaka mmoja au zaidi.+ Tangu siku aliyokimbilia kwangu mpaka leo sijampata na kosa lolote.”