21 Halafu Abneri akamwambia Daudi: “Acha niende nikawakusanye pamoja Waisraeli wote kwako bwana wangu mfalme, ili wafanye agano pamoja nawe, nawe utakuwa mfalme juu ya kila kitu upendacho.”* Basi Daudi akamruhusu Abneri aende, akaenda zake kwa amani.