5 Yehonadabu akamwambia: “Lala kitandani mwako, ujifanye mgonjwa. Baba yako akija kukuona, mwambie, ‘Tafadhali, mruhusu dada yangu Tamari aje kuniandalia chakula kidogo. Akitayarisha chakula cha mgonjwa mbele ya macho yangu nitakichukua kutoka mkononi mwake na kula.’”