10 Kisha Amnoni akamwambia Tamari: “Niletee chakula* katika chumba cha kulala, ili nikichukue kutoka mkononi mwako na kukila.” Basi Tamari akachukua keki zenye umbo la moyo ambazo alikuwa ameoka na kumletea Amnoni ndugu yake katika chumba cha kulala.