7 Sasa inuka, toka nje ukawatie moyo watumishi wako, kwa sababu naapa kwa jina la Yehova kwamba usipotoka nje, hakuna mtu atakayebaki pamoja nawe usiku wa leo. Hili litakuwa jambo baya zaidi kwako kuliko madhara yote yaliyokupata tangu ulipokuwa kijana mpaka sasa.”