18 Ndipo Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imebaki katika hazina za nyumba ya Yehova na hazina za nyumba ya mfalme na kuwapa watumishi wake. Kisha Mfalme Asa akawatuma kwa Ben-hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Siria,+ aliyekuwa akiishi Damasko, akamwambia: