14 Kwa hiyo Mfalme Hezekia wa Yuda akatuma ujumbe huu kwa mfalme wa Ashuru kule Lakishi: “Nimekosea. Ondokeni, msinishambulie, nami nitalipa chochote mtakachonitoza.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Mfalme Hezekia wa Yuda faini ya talanta 300 za fedha na talanta 30 za dhahabu.