32 mpaka nitakapokuja na kuwapeleka katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe,+ nchi yenye nafaka na divai mpya, nchi yenye mikate na mashamba ya mizabibu, nchi yenye mizeituni na asali. Ndipo mtakapoishi, nanyi hamtakufa. Msimsikilize Hezekia, kwa maana anawapotosha kwa kusema, ‘Yehova atatuokoa.’