26 Ndipo akamwambia: “Je, moyo wangu haukuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukupokea? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea mavazi au mashamba ya mizeituni au mashamba ya mizabibu au kondoo au ng’ombe au watumishi wa kiume au watumishi wa kike?+