5 Basi msimamizi wa jumba la mfalme, gavana wa jiji, wazee, na wale walezi wakamtumia Yehu ujumbe huu: “Sisi ni watumishi wako, nasi tutafanya mambo yote utakayotuambia. Hatutamweka yeyote kuwa mfalme. Fanya jambo lolote unaloona ni jema machoni pako.”