14 Kisha akamwona mfalme akiwa amesimama hapo kando ya nguzo kama ilivyokuwa desturi.+ Wakuu na wapiga tarumbeta+ walikuwa pamoja na mfalme, na watu wote nchini walikuwa wakishangilia na kupiga tarumbeta. Ndipo Athalia akayararua mavazi yake na kupaza sauti: “Ni njama! Ni njama!”