41 Watu hao ambao majina yao yameorodheshwa walikuja katika siku za utawala wa Mfalme Hezekia+ wa Yuda, wakayabomoa mahema ya Wahamu na Wameunimu waliokuwa huko. Waliwaangamiza tangu siku hiyo; wakachukua eneo lao kwa sababu lilikuwa na malisho kwa ajili ya wanyama wao.