23 Mfalme Yehoashi wa Israeli akamkamata Mfalme Amazia wa Yuda, mwana wa Yehoashi mwana wa Yehoahazi, huko Beth-shemeshi. Kisha akamleta Yerusalemu, naye akabomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu+ mpaka Lango la Pembeni,+ urefu wa mikono 400.