10 Pia, alijenga minara+ nyikani na kuchimba matangi mengi ya maji (kwa maana alikuwa na mifugo mingi sana); alifanya hivyo pia katika Shefela na katika nchi tambarare ya juu. Alikuwa na wakulima na watunzaji wa mizabibu milimani na kule Karmeli, kwa maana alipenda kilimo.