15 Pia, alitengeneza mitambo ya vita huko Yerusalemu iliyobuniwa na wahandisi; iliwekwa kwenye minara+ na kwenye pembe za kuta, nayo ilikuwa na uwezo wa kurusha mishale na mawe makubwa. Basi umaarufu wake ukaenea kwa mapana na marefu, kwa maana alisaidiwa sana akawa na nguvu.