-
2 Mambo ya Nyakati 28:15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Kisha wanaume waliokuwa wamechaguliwa na kutajwa majina wakaenda na kuwachukua mateka, nao wakachukua mavazi kutoka katika zile nyara na kuwapa wote waliokuwa uchi. Basi wakawavika mavazi na kuwapa viatu, vyakula na vinywaji, na mafuta ya kujipaka. Zaidi ya hayo, waliwasafirisha kwa punda watu waliokuwa dhaifu na kuwapeleka kwa ndugu zao kule Yeriko, jiji la mitende. Kisha wakarudi Samaria.
-