8 Tungependa kumjulisha mfalme kwamba tulienda katika mkoa wa Yuda kwenye nyumba ya yule Mungu mkuu, nayo inajengwa kwa mawe makubwa yaliyobingirishwa na kuwekwa mahali pake, na mbao zinawekwa katika kuta. Watu hao wanafanya kazi hiyo kwa bidii na inasonga mbele kwa jitihada zao.