18 Kila siku nilitayarishiwa ng’ombe dume mmoja, kondoo sita walio bora, na ndege wengi, na kila baada ya siku kumi tuliandaliwa kwa wingi divai ya kila aina. Licha ya hayo sikudai chakula kilichokuwa haki ya gavana, kwa kuwa tayari watu walikuwa wamelemewa na kazi.