3 Na mfalme ateue wajumbe katika mikoa yote ya milki yake+ ili wawakusanye pamoja na kuwaleta wasichana wote warembo walio mabikira kwenye nyumba ya wanawake katika ngome ya Shushani. Watatunzwa na Hegai+ towashi wa mfalme aliye mlinzi wa wanawake, nao watarembeshwa.