15 Ilipofika zamu yake ya kuingia kwa mfalme, Esta binti ya Abihaili ndugu ya baba ya Mordekai, aliyemchukua na kumlea kama binti yake,+ hakuomba chochote ila vitu alivyopendekeza Hegai towashi wa mfalme, aliyekuwa mlinzi wa wanawake. (Wakati wote huo kila mtu aliyemwona Esta alipendezwa naye.)