3 “Nimelikanyaga pipa la divai nikiwa peke yangu.
Hakuna mtu yeyote kutoka katika mataifa aliyekuwa pamoja nami.
Niliendelea kuwakanyaga kwa hasira yangu,
Nami niliendelea kuwakanyaga kwa ghadhabu yangu.+
Mavazi yangu yalijaa madoa ya damu yao,
Nami nimezichafua nguo zangu zote.