22 Lakini, baadhi ya watu waliobaki humo wataponyoka na kutolewa nje,+ wana na mabinti. Wanakuja kwenu, nanyi mtakapoona njia zao na matendo yao, kwa hakika mtafarijiwa kuhusiana na msiba ambao nilileta dhidi ya Yerusalemu, kuhusu kila jambo ambalo nilitenda dhidi ya jiji hilo.’”