16 Nitayafanya mataifa yatetemeke kwa sauti ya kuanguka kwake nitakapoushusha Kaburini pamoja na wote wanaoshuka shimoni, na miti yote ya Edeni,+ miti iliyo bora na iliyo mizuri kabisa ya Lebanoni, miti yote iliyonyweshwa maji mengi, itafarijiwa katika nchi iliyo chini.