2 “Mwana wa binadamu, mwimbie wimbo wa huzuni mfalme Farao wa Misri, nawe umwambie,
‘Ulikuwa kama mwanasimba mwenye nguvu wa mataifa,
Lakini umenyamazishwa.
Ulikuwa kama mnyama mkubwa sana wa baharini,+ ukitibua maji katika mito yako,
Ukivuruga maji kwa miguu yako na kuchafua mito.’