30 “‘Wakuu wote wa kaskazini wako huko, pamoja na Wasidoni wote,+ ambao wameshuka kwa aibu pamoja na waliouawa, ingawa walisababisha hofu kwa nguvu zao. Watalala wakiwa hawajatahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga nao watabeba aibu yao pamoja na wale wanaoshuka chini shimoni.