10 Lakini ofisa mkuu wa makao ya mfalme akamwambia Danieli: “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, ambaye ametoa maagizo kuhusu vyakula na vinywaji vyenu. Itakuwaje akiona kwamba afya yenu ni mbaya kuliko ya vijana wengine wa rika lenu? Mtanifanya niwe na hatia mbele ya mfalme.”